EBOLA- UGONJWA WA AJABU USIO NA TIBA.
EBOLA- UGONJWA WA AJABU USIO NA TIBA.
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi.
Tambua jinsi Ebola inavyoweza kuenezwa.
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kama Homa za virusi zinazosababisha kutoka Damu mwilini.
Ugonjwa huu unaathiri binadamu na wanyama kama vile nyani, ngedere, sokwe na popo.
1. Ugonjwa wa Ebola ni nini?
⦁ Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa.
⦁ Shirika la afya duniani, ⦁ WHO linasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan.
⦁ Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya (Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho,kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa.
2. Binadamu anaambukizwa vipi kirusi cha Ebola?
Maambukizi hutokea pindi mtu anapoambukizwa kupitia sehemu wazi ya mwili wake kugusana na majimaji ya mgonjwa wa Ebola.
Mathalani;
⦁ matapishi
⦁ choo
⦁ mate
⦁ mbegu za kiume, au Semen
⦁ na damu. Maambukizi yanaweza kutokea pia iwapo ngozi yenye uwazi ya mtu asiye na ugonjwa huo itakumbwa na maji maji yenye kirusi yaliyomo kwenye nguo chafu za mgonjwa, mashuka au sindano zilizotumika.
Dondoo;
⦁ Mtu anaweza kuambukiza kirusi cha Ebola iwapo damu yake au majimaji ya mwilini yana kirushi hicho.
⦁ Mgonjwa wa Ebola anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa hali ya juu kutoka kwa wataalamu na wafanyiwe uchunguzi kuhakikisha kirusi hakipo tena mwilini kabla ya kurejea nyumbani.
⦁ Mtaalamu wa afya baada ya kipimo anabaini kuwa mgonjwa ni salama kurejea nyumbani kwa kuwa amepona na hana tena kirusi, hawezi kuambukiza wengine.
Angalizo;
⦁ Wanaume ambao wamepona ugonjwa huo bado wanaweza kuambukiza kupitia njia ya kujamiiana ndani ya wiki saba baada ya kupona.
⦁ Wanaume wanashauriwa kutoshiriki tendo hilo ndani ya wiki saba baada ya kupona. Na iwapo atalazimika basi atumie mpira wa kiume.
3. Nani yuko hatarini zaidi?
Wakati wa mlipuko, walio hatarini zaidi kuambukizwa ugonjwa wa Ebola ni:
⦁ Wahudumu wa afya;
⦁ Wanafamilia au watu wengine walio karibu na mgonjwa wa Ebola
⦁ Waombolezaji ambao wanashika maiti ya mgonjwa wa Ebola kama sehemu ya ibada ya mazishi.
4. Dalili za Ebola ni zipi?
⦁ Homa ya ghafla
⦁ Uchovu wa kina
⦁ Maumivu ya misuli
⦁ Maumivu ya kichwa
⦁ Koo kukauka.
⦁ Kutapika
⦁ Kuhara
⦁ Vipele
⦁ Figo kushindwa kufanya kazi
⦁ Halikadhalika ini
⦁ Damu kuanza kuvuja ndani na nje ya mwili.
Baada ya dalili hizo kuonekana, ugonjwa unaweza kubainika kati ya siku Mbili hadi 21 na hapo ndipo mgonjwa anaweza kuambukiza wengine. Wakati ugonjwa haujabainika, mtu hawezi kuambukiza mtu mwingine.
Thibitisho la ugonjwa huu hupatikana maabara pekee baada ya kufanyiwa vipimo.
5. Je kuna tiba au chanjo?
Kwa sasa hakuna dawa au chanjo iliyosajiliwa kutibu ugonjwa wa kirusi cha Ebola. Hata hivyo dawa kadhaa zinaendelezwa na WHO imeridhia tiba ya majaribio kutumika kutibu wagonjwa.
6. Angalizo
Wahudumu wa afya wanaweza kukumbana na mazingira yenye majimaji kutoka mwili wa mgonjwa wa Ebola pindi wanapokuwa wanatoa huduma kwa wagonjwa hao.
⦁ Hii hutokea iwapo hawana mavazi stahili ya kujikinga au hawakuzingatia taratibu za kujikinga pindi wanapohudumia wagonjwa.
⦁ Haishauriwi familia au jamii kuhudumia wagonjwa wanaoweza kuwa na dalili za Ebola majumbani mwao.
⦁ Huduma kwa mgonjwa wa Ebola zitolewe hospitali au kituo cha afya.
⦁ Maambukizi mengine yameripotiwa kwenye mazishi au mila za mazishi.
⦁ Waombolezaji kwenye msiba wa mgonjwa wa Ebola waponagusana na mwili wa marehemu hujiweka kwenye hatari ya maambukizi.
WHO inasihi mazishi ya waliofariki dunia kwa Ebola yafanyike kwa kiwango kikubwa cha kujikinga kwa kuvaa mavazi maalum na wanaofariki dunia wazikwe mara moja.
Mazishi yafanyike chini ya usimamizi wa wataalamu wa afya na serikali ya nchi husika.
Muhimu.
⦁ Epuka kugusana na mgonjwa wa Ebola.
⦁ Epuka kula nyama ya mnyama pori aliekufa/ kuuawa porini
⦁ zifahamu kwa ufasaha dalili zote za ugonjwa wa Ebola
⦁ Nawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na tumia sabuni mara kwa mara.
⦁ Valia mavazi ya kujikinga uwapo karibu na mgonjwa wa Ebola- muhimu kwa wahudumu wa afya na ndugu.

Comments
Post a Comment